Hakikisho la Kipekee la Mfululizo wa Waamuzi wa Mwisho
NA HUMPHREY MTANDWA
ENOKI alitabiri na kuzungumzia waamuzi watakaoinuliwa katika nyakati zetu. Alizungumzia jinsi watakavyouhukumu ulimwengu kwa dhambi zake. Wanaume na wanawake hawa wanabeba Roho Mtakatifu na kwa Roho Mtakatifu wanauthibitishia ulimwengu kwa dhambi zake.
Ili kuwa mwamuzi, mamlaka lazima yawe juu yako na yanatolewa kupitia ujuzi wa maandiko. Watu hawa wana uelewa wa Neno la Mungu na wamelijua Neno sana kiasi kwamba wamekuwa kitu kimoja na Neno lenyewe.
Neno na Roho vinamstahilisha mtu kuwa mwamuzi. Lazima kuwe na usawa kati ya Neno la Mungu na Roho Wake Mtakatifu. Katika wakati wetu wale wanaomdhihirisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wake baadhi yao hawajui maandiko na wale wanaojua Maandiko hawaonyeshi nguvu za Roho Mtakatifu, lazima kuwe na usawa. Lazima ujue neno na Roho. Ukijua kanuni hii uwezo wako unaongezeka na pia nafasi yako kama mwamuzi. Kadiri mwanga ulivyo mkubwa, ndivyo hukumu na utekelezaji wa mtu unavyokuwa sahihi zaidi.
Giza hutoweka nuru inapoangaza, sisi kama waamuzi tunaingiza nuru katika eneo lolote la giza. Giza linaweza kuwa chochote kinachopingana na Neno la Mungu. "Lakini mtu wa rohoni huyahukumu yote, wala yeye hahukumiwi na mtu." (1 Wakorintho 2:15).
Ni kupitia macho ya Neno la Mungu mtu huhukumu. Ni Neno linalomfanya mtu kuwa wa kiroho. Linampa mtu utambuzi. Lakini hakuna mtu anayeweza kumhukumu mteule kwa sababu hawana kifaa cha kufanya hivyo. Kifaa hicho ni Neno la Mungu. Neno ni nuru. Ni nuru ile ambayo mtu hubeba ambayo hupita katika hali zinazomfanya mtu kuwa mwamuzi. Wengi hawabebi Neno, kwa hivyo hawawezi kuleta utaratibu wa Mungu kwa ulimwengu. Mwamuzi hubeba nuru inayofichua giza na asili ya yule mwovu. Magonjwa, umaskini, njaa, hofu, maumivu - haya yote yanaweza kuhukumiwa, lakini kupitia Neno la Mungu pekee.
Kanisa bado halijajua kikamilifu msimamo wake na kwa sababu baadhi bado ni wahanga wa mifumo ya ulimwengu, katika kitabu chake kinachoitwa, The Godman, Nabii Tanya Jeriel anasema Mungu hazungumzi Kiingereza na anaendelea kuelezea sauti ya Mungu. Waumini wengi hawajui sauti ya Mungu. Wangependelea mtu awaelezee uzoefu wake na tafsiri yake ya maandiko. Anaendelea kusema, “Musa alitamani kusikia sauti ya Mungu, lakini wana wa Israeli waliiogopa.” Waumini wengi hawajui jinsi ya kuhusianisha na Mungu.
Kanisa la leo halijaelewa kikamilifu msimamo wake na isipokuwa likiamka na kuona ukweli huu, huenda lisiweze kuhukumu ulimwengu na kuufanya ulimwengu utiishwe chini ya mapenzi ya Mungu. Sisi ni jeshi la alfajiri, lakini katika safu za jeshi hili, hatupaswi kuwa watoto wachanga, bali waumini waliokomaa ambao wanaweza kushughulikia Neno la Mungu na kulitumia vizuri kuhukumu ulimwengu wenyewe kuhusu dhambi zake.
Mungu akubariki.